MAFUNZO YA KOZI FUPI! - USIMAMIZI WA KUMBUKUMBU KATIKA MAZINGIRA YA KIDIJITALI
MAFUNZO YA KOZI FUPI! - USIMAMIZI WA KUMBUKUMBU KATIKA MAZINGIRA YA KIDIJITALI
TANGAZO: WITO WA KUSHIRIKI MAFUNZO YA MUDA MFUPI YA USIMAMIZI WA KUMBUKUMBU KATIKA MAZINGIRA YA KIDIGITALI
BAGAMOYO, TANZANIA – Chuo cha Usimamizi wa Maktaba, Nyaraka na Kumbukumbu (SLADS), kilicho chini ya Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB), kinawakaribisha watumishi kutoka sekta ya umma na binafsi, watafiti, na wadau wote wanaovutiwa, kuomba kushiriki katika mafunzo maalum ya muda mfupi.
Ratiba ya mafunzo hayo ni kama ifuatavyo:
Jina la Kozi: Records Management Practices in the Digital Environment (Usimamizi wa Kumbukumbu katika Mazingira ya Kidigitali)
Tarehe: Tarehe 22 hadi 26 Juni, 2026
Mahali: Hoteli ya Stella Maris, Bagamoyo
Malengo ya Mafunzo
Kozi hii imelenga kuwajengea washiriki ujuzi wa kisasa kuhusu usimamizi wa kumbukumbu katika mazingira ya kidigitali, matumizi ya teknolojia katika utunzaji wa taarifa, pamoja na mbinu bora za usimamizi wa nyaraka za kielektroniki ili kuongeza ufanisi, uwazi na tija katika utendaji kazi wa kila siku serikalini na katika sekta binafsi.
Walengwa wa Mafunzo
Katika kuunga mkono jitihada za kitaifa za mabadiliko ya kidigitali na uwajibikaji kitaasisi, mafunzo haya yanashauriwa kwa:
Maafisa Usimamizi wa Kumbukumbu na Nyaraka (Records and Archives Management Officers)
Wasaidizi wa Usimamizi wa Kumbukumbu na Nyaraka katika masijala za taasisi za umma na binafsi
Wanafunzi wa Ngazi ya Uzamili (Postgraduate) na Watafiti wa Kitaaluma
Mtaalamu au mdau yeyote anayehusika na usimamizi wa data na nyaraka za taasisi
Usajili na Mawasiliano
Kwa ajili ya uteuzi wa washiriki kutoka taasisi, kuthibitisha nafasi, au kwa ufafanuzi zaidi wa kiofisi, tafadhali wasiliana na waratibu wa mafunzo kupitia njia zifuatazo:
Bw. Leonard Kibuti (Mratibu wa Mafunzo) – Simu: 0744539658
Bibi. Irene Malewa (Mratibu wa Mafunzo) – Simu: 0615237974
Barua Pepe Rasmi: slads@tlsb.go.tz au management@slads.ac.tz
Limetolewa na:
Uongozi,
Chuo cha Usimamizi wa Maktaba, Nyaraka na Kumbukumbu (SLADS).

