Dira na Dhima

Dira
Dira ya Chuo ni:
Kuwa taasisi ya mafunzo ya umahiri kwa katika fani ya Ukutubi, Usimamizi wa Nyaraka, Usimamizi wa Kumbukumbu na Utaalamu wa Habari barani Afrika.

Dhima ya Chuo
Kuboresha elimu ya Sayansi ya Maktaba na Habari kupitia mafunzo na utafiti.

Malengo ya Chuo
a. Kutoa  mafunzo katika fani za Ukutubi, Habari, Usimamizi wa Nyaraka, Usimamizi wa Kumbukumbu na Masomo ya Uandishi wa Nyaraka katika viwango vya NTA 4, 5 na 6.
b. Kutoa elimu endelevu ya Maktaba, Usimamizi wa Nyaraka, Usimamizi wa Kumbukumbu na Utaalamu wa Habari nchini Tanzania.
c. Kukuza na kufanya utafiti katika fani za Maktaba, Usimamizi wa habari, Usimamizi wa Nyaraka na Usimamizi wa Kumbukumbu.
d. Kuchapisha maandiko ya  kujifunzia katika fani za Maktaba, Usimamizi wa habari, Nyaraka na Usimamizi wa Kumbukumbu.
e. Kutoa huduma za ushauri katika kupanga, kuanzisha na kuendeleza maktaba, vituo vya usimamizi wa nyaraka, Usimamizi wa kumbukumbu na vituo vya habari.