Tafiti
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka na Mkurugenzi Mkuu wa TLSB Dkt. Mboni Ruzegea, leo tarehe 11 Machi, 2025 amefungua Mkutano wa Wadau kwa kuhakiki Mtaala wa Chuo cha SLADS. Katika hotuba yake, Dkt. Ruzegea amewataka washiriki wa Mkutano huo kusikiliza kwa makini wasilisho la Mtaala huo na kujadili namna bora itakayosaidia kumwezesha mwanafunzi kuwa na ujuzi, kuwa Mjasiriamali na mtunza kumbukumbu na takwimu (data).vilevile, amewataka kuhakikisha wanajadili namna bora ya Mtaala utakavyomfanya mwanafunzi na Jamii kwa ujumla kujenga utamaduni wa kujisomea (Reading Culture). Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi na Mwenyekiti wa Baraza, Kaimu Mkuu wa chuo cha SLADS Bi. Bertha Mwaihojo alieleza kuwa dhumuni la Mkutano huo ni kuwashirikisha Wadau ili kwa pamoja wahakiki Mtaala na kupata mawazo, ushauri na maboresho zaidi kwenye Mtaala huo. Aidha.

