MAFUNZO YA KOZI FUPI! - MATUMIZI YA MSINGI YA KOMPYUTA NA USIMAMIZI WA TAARIFA ZA KIELEKTRONIKI
MAFUNZO YA KOZI FUPI! - MATUMIZI YA MSINGI YA KOMPYUTA NA USIMAMIZI WA TAARIFA ZA KIELEKTRONIKI
TANGAZO: WITO WA KUSHIRIKI MAFUNZO YA MUDA MFUPI YA MATUMIZI YA MSINGI YA KOMPYUTA NA USIMAMIZI WA TAARIFA ZA KIELEKTRONIKI
BAGAMOYO, TANZANIA – Chuo cha Usimamizi wa Maktaba, Nyaraka na Kumbukumbu (SLADS), kilicho chini ya Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB), kinawakaribisha wananchi, watumishi wa sekta ya umma na binafsi, na wadau wote kuomba kushiriki katika mafunzo ya muda mfupi ya Matumizi ya Msingi ya Kompyuta na Usimamizi wa Taarifa za Kielektroniki (Digital Information Management).
Ratiba na maelezo ya mafunzo hayo ni kama ifuatavyo:
Muda wa Mafunzo: Wiki Nne (4) (Kuanzia tarehe 23 Juni hadi 23 Julai, 2026)
Mwisho wa Kutuma Maombi: Tarehe 20 Juni, 2026
Ada ya Mafunzo: Tsh 150,000/=
Mahali: Kampasi ya SLADS, Bagamoyo
Muundo wa Mafunzo
Mafunzo haya yamelenga kuwajengea washiriki ujuzi thabiti wa kiteknolojia katika maeneo yafuatayo:
Utangulizi wa Mifumo ya Kompyuta (Introduction to Computer Systems)
Matumizi ya Programu za Microsoft Office (Word, Excel, PowerPoint, n.k.)
Matumizi ya Mtandao na Mawasiliano ya Kielektroniki (Internet & Digital Communication)
Usimamizi wa Taarifa za Kielektroniki (Digital Information Management)
Ulinzi wa Data na Usalama wa Mtandao (Data Security & Cyber Safety)
Walengwa wa Mafunzo
Mafunzo haya yanajumuisha mtu yeyote anayetaka kuongeza ujuzi wa vitendo katika teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA), wakiwemo wafanyakazi wa maofisini, wahitimu wa shule/vyuo, na jamii kwa ujumla.
TAARIFA KWA UMMA: Chuo (SLADS) kinapenda pia kuwajulisha wananchi kuwa usajili wa masomo kwa ngazi ya Stashahada ya TEHAMA (Diploma in ICT) na Stashahada ya BICT kwa mwaka wa masomo 2026/2027 sasa upo wazi.
Taratibu za Usajili na Mawasiliano
Kwa ajili ya uthibitisho wa nafasi au kwa ufafanuzi zaidi wa kiofisi, tafadhali wasiliana na waratibu wa mafunzo kupitia:
Bw. Leonard Kibuti – Simu: 0744539658
Bibi. Irene Malewa – Simu: 0615237974
Barua Pepe Rasmi: slads@tlsb.go.tz au management@slads.ac.tz
Limetolewa na:
Uongozi,
Chuo cha Usimamizi wa Maktaba, Nyaraka na Kumbukumbu (SLADS).

