Maelezo Mafupi

Kampasi ya Bagamoyo ni miongoni mwa Kampasi mbili za Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka. Kampasi ya Bagamoyo ilianzishwa rasmi mwaka 1989 ikiwa ni kampasi ya kwanza kuanzishwa kati ya Kampasi mbili za Chuo. Kuanzishwa kwa Kampasi ya Bagamoyo ni utekelezaji wa Sheria ya uanzishwaji wa Bodi ya huduma za maktaba Tanzania. Kampasi ya Bagamoyo ipo Barabara ya Bagamoyo, Kata ya Dunda mtaa wa Ukuni wilaya ya Bagamoyo.