Maelezo Mafupi
Kampasi ya Dar es salaam ni miongoni mwa Kampasi mbili za Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka. Kampasi ya Dar es salaam ilianzishwa rasmi mwaka 1989 ikiwa ni kampasi ya pili kuanzishwa kati ya Kampasi mbili za Chuo. Kuanzishwa kwa Kampasi ya Dar es salaam ni utekelezaji wa Sheria ya uanzishwaji wa Bodi ya huduma za maktaba Tanzania. Kampasi ya Dar es salaam ipo Barabara ya Bibi Titi Mohamed,
wilaya ya Ilala, Dar es salaam.

